KITIMLA AJITOSA KUWATUMIKIA WANANCHI JIMBO LA KIGAMBONI

 


Mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mkazi wa Kigamboni, Sinan Seif Kitimla, amejitosa rasmi katika kinyang’anyiro cha ubunge wa Jimbo la Kigamboni, jijini Dar es Salaam.

 

Kitimla amechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo Juni 28, 2025 ikiwa ni siku ya kwanza ya kuanza kwa zoezi la uchukuaji wa fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kupitia CCM nchini kote. Zoezi hilo linatarajiwa kufungwa rasmi Julai 2, 2025.

 

Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu, Kitimla amesema amejiandaa kuwatumikia wananchi wa Kigamboni kwa kuzingatia mahitaji yao halisi na kuhakikisha maendeleo jumuishi katika sekta mbalimbali. Ametoa wito kwa wanachama wenzake na wakazi wa jimbo hilo kumuunga mkono katika safari hii ya kisiasa.

 

Zoezi la kuchukua na kurejesha fomu linaendelea katika ngazi zote za chama huku wagombea wakihimizwa kuzingatia taratibu, kanuni na maadili ya uchaguzi ndani ya CCM.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv


Post a Comment

0 Comments