TANESCO KINARA TENA UBORA WA HUDUMA KWA WATEJA CICM

 



Uboreshaji wa kutumia njia za kidigitali kurahisisha mchakato wa maombi ya umeme na upatikanaji wa huduma kuwa mwepesi kwa wateja wake walipatia Shirika la umeme Tanzania TANESCO kwa mara nyingine tena ushindi wa tuzo ya the ''Most improved Organization'' eneo la huduma kwa wateja iliyotolewa na Taasisi ya Chartered Institute of Customer Management(CICM) Machi 28,2025 jijini Dar es Salaam.

 

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja Bi Irene Gowelle kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO amesema, Tuzo hizo ni heshima kwa Shirika ikiwa ni ishara nzuri ya uboreshaji unaofanyika kutambuliwa na kuthaminiwa.

 

‘’Tuzo hizi ni heshima kubwa kwa TANESCO, zinatuongezea ari ya kufanya vizuri zaidi, tutaongeza ubunifu katika utoaji wa huduma bora kwa wateja wetu’’

 

Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Mha. Gissima Nyamo-Hanga na yeye ameshinda Tuzo ya heshima ya Kiongozi anayefanya mabadiliko chanya yenye tija upande wa huduma kwa wateja katika Sekta ya Umma.

 

Tuzo za Tanzania Service excellence awards hutolewa kila mwaka na zinalenga kutambua Taasisi za Umma na binafsi zinazoimarisha na kuboresha huduma bora kwa wateja wake.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments