Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki Baraza la Eid El-Fitr na kuzungumza na Waumini wa Dini ya Kiislamu pamoja na wageni mbalimbali katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam , Machi 31, 2025,
Aidha, Rais Samia amewasihi viongozi wa dini kushikilia msimamo wa imani, udhibiti wa nafsi na wajibu katika kuikuza na kuitunza amani nchini, pia amewaomba viongozi wa dini kuwadhibiti wale wachache miongoni mwao walio na muelekeo wa kuhubiri na kupandikiza chuki kwa wananchi dhidi ya serikali yao.
Pia amesisitiza kuwa, ni vyema kujua kuwa katika mifarakano na hasama hakuna atakayeibuka mshindi bali kutatokea hasara na majanga, ameongeza kuwa, Jukumu la kusimamia amani nchini ni la serikali kupitia vyombo vya ulinzi na usalama, kwa upande mwengine ni jukumu la wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ameongeza kuwa kwa kiasi kikubwa ari na mori za wananchi huchochewa na maelekezo ya viongozi wao wa dini, hivyo kwa msingi huo amewiwa kulitupa jukumu la amani na utulivu nchini kwa viongozi wa dini.
Vilevile Rais Dkt. Samia ameweka wazi kuwa, Serikali kwa upande wake itasimamia na kulinda misingi ya katiba na kuheshimu uhuru wa raia kuabudu na kuhubiri dini, ila kamwe haitomvumilia yeyote atakayevunja haki hii kuchochea chuki na uhasama nchini.
"Tumeapa kulinda haki na utu wa kila Mtanzania, hivyo hatutosita kufanya wajibu wetu bila woga, waswahili husema, chelea mwana kulia basi hulia yeye, hivyo hatutoacha mwana atovuke ili kulinda wengi wasilie, Serikali haitofanya ajizi ya kutokushugulika na wavunjifu wa amani na wachochezi wa vurugu.
"Dini ibaki katika majukumu yake ya msingi ya kulea waumini kiroho na kimaadili, na viongozi wa dini wasidandie ajenda au vishawishi vya siasa. Matarajio ya serikali ni kwamba viongozi wa dini." Amesisitiza Rais Dkt. Samia.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments