Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango, amezindua mbio za Mwenge wa Uhuru 2025, katika viwanja vya shirika la elimu Kibaha mkoani Pawani.
Uzinduzi huo uliofanyika leo Aprili 2, 2025 umehudhiriwa na baadhi ya viongozi wa Kitaifa akiwemo Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko na Rais Mstaafu wa awamu ya Nnne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Sherehe hizo zimeongozwa na kauli mbiu: “ Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu”.
Viongozi wengine ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Zungu, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments